Baraza kuu la makanisa nchini (NCCK) limeonya kuhusu uwezekano wa kuhairishwa kwa uchaguzi kuu wa 2022.

Kupitia kwa katibu mkuu Chris Kinyanjui, NCCK inahoji kwamba uchaguzi huo ni sharti uandaliwe Agosti mwaka ujao kulingana na katiba na kwamba kuhairishwa kutasababisha mtafaruku wa kisiasa nchini.

Kinyanjui amesema haya alipohutubia kongamano la wajumbe katika eneo la Pwani ambapo amewataka wanasiasa kukoma kutumia madhabahu kupiga siasa.

Msimamo wa NCCK unawadia baada ya katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli kuashiria kwamba uchaguzi huo utahairishwa iwapo mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI utakwama.