Tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma (SRC) imesimamisha utathmini wa mishahara na marupurupu ya watumishi wote wa umma kwa muda wa miaka miwili ijayo.

Mwenyekiti wa SRC Lyn Mengich amesema pendekezo hilo limetolewa na wizara ya fedha ikitaja hali ngumu ya kiuchumi iliyosababishwa na janga la corona.

Amesema kwa sasa kiasi kikubwa cha pesa kinatumika kulipa mishahara ya watumishi wa umma wakati ambapo uchumi unakumbwa na hali ngumu tangu kulipuka kwa janga hilo.

Mara ya mwisho kwa watumishi wa umma kuongezewa mishahara ilikuwa na Julai 1, 2020.