Wazazi wametakiwa kuridhika na shule walizopata wanao waliokalia mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE.

Akizungumza akiwa Thika leo, waziri wa elimu Profesa George Magoha ametetea zoezi la uteuzi lililokamilika juzi licha ya baadhi ya wazazi kulalamikia shule walizopata wanao.

Malalamishi ya wazazi hao ni kwamba zoezi hilo halikuwa na haki.

Wanafunzi hao wanatazamiwa kuripoti katika shule zao Agosti 2.