Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini (COTU) Francis Atwoli amesema huenda uchaguzi mkuu wa 2022 ukahairishwa iwapo mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI hautakuwa umekamilika.
Atwoli ameashiria kwamba upo uwezekano wa kuhairisha uchaguzi huo angalau kwa mwaka moja iwapo wabunge watashawishika kufanya hivyo.
Atwoli vile vile amewataja kama wenye wivu watu walioharibu bango lenye jina lake katika eneo la Kileleshwa akisema walioamua kuita barabara kwa jina lake walifanya hivyo kutambua mchango wake.