Wizara ya Afya imekiri kuna upungufu wa chanjo dhidi ya virusi vya corona kufuatia lalama zilizoibuliwa na muungano wa madaktari.

Kupitia kwa mtandao wa Twitter, wizara hiyo chini ya uongozi wa Mutahi Kagwe imekiri kuwa wahudmu wa Afya na wakenya wengine wamekuwa wakienda kupokea dozi ya pili katika vituo vya afya vilivyotengewa lakini wakaishia kurejea nyumbani bila.

Wizara hiyo hata hivyo inatoa hakikisho kwa wakenya kuwa chanjo ziadi zitawasili humu nchini hivi karibuni na kwamba wote waliopata dozi ya kwanza, watapokea na ya pili.

Wizara hiyo inawataka wahudumu wa Afya na wakenya wengine wanaotegea dozi ya pili kuwa na subira na kuongeza kuwa wahudumu wa Afya watapewa kipaumbele katika dozi hiyo ya pili pindi chanjo zaidi zitawasili nchini.