Wanafunzi waliokalia mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wa mwaka 2020 watajiungfa na kidato cha kwanza tarehe mbili mwezi wa nane mwaka huu.
Waziri wa Elimu profesa George Magoha amesema wanafunzi wote waliofanya mtihani huo watajiunga na shule za upili huku mwanafunzi wa kwanza Faith Mumo akijiunga na shule ya Kenya High huku mwanafunzi bora wa kiume Samuel Wanyonyi akijiunga na shule ya upili ya Mangu.
Kuhusiana na mipango ya kujiandaa kufanikisha mtaala mpya wa elimu, CBC, Magoha amesema wanaendelea kutengeneza madawati zaidi ambayo yatapelekwa katika shule zinazotumika kutoa mafunzo hayo.
Wanafunzi wanaweza kufahamu shule walizochaguliwa kujiunga nazo kupitia kwa mtandao au kutuma nambari za usjaili wa mitihani (Index Number) kwa 22263
Mtihani huo ulifaa kufanyika mwishoni mwa mwaka uliopita lakini ukahairishwa hadi mwaka huu kutokana na janga la covid-19.