Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imelalamikia kukosa pesa za kutosha kufanikisha shughuli zake kikamilifu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati wake kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema kunafaa kuwa na sheria ili kuhakikisha kwamba wanapata pesa za kutosha na wala sio wakati wa uchaguzi pekee.

Chebukati ametaja kwamba kutakuwa na zaidi ya sava moja kwa ajili ya kupeperusha matokeo wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Kwenye bajeti iliyowasilishwa bungeni juma lililopita, IEBC ilitengewa Sh14.5b na wizara ya fedha kwa minajili ya maandalizi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.