Polisi huko Kericho wanamtafuta mwanafunzi wa kidato cha tatu anayedaiwa kumpiga hadi kumuua babake kwa madai ya kuuza kuku wake.

Akidhibitisha tukio hilo, chifu wa kijiji cha Barotion huko Londiani amesema kwamba malumbano yalianza wakati kijana huyo alirejea nyumbani na kupata jogoo wake alikuwa ameuzwa bila yeye kuulizwa.

Mshukiwa alikasirishwa na majibu ya babake aliyemwambia kuwa jogoo huyo hayuko na kumshambulia kwa kifaa butu na kumuumiza.

Juhudi za majirani kuokoa maisha ya baba huyo kwa kumkimbiza hospitalini hazikufaulu kwa sbabau alifariki kutokana na majeraha akipokea matibabu.