Mfanyibiashara maarufu Dr. Chris Kirubi amefariki dunia, imedhibitisha familia yake.

Dj CK alivyofahamika na wengi hata kwenye ulimwengu wa redio amefariki akiwa na umri wa miaka 80 baada ya mapambano ya muda mrefu na ugonjwa wa Saratani.

Taarifa kutoka kwa familia yake imearifu kuwa Chris Kirubi alikata roho mwendo wa saa saba za mchana Jumatatu baada ya vita vya muda mrefu na saratani ambapo alionesha ukakamavu.

Marehemu ambaye amekuwa akipambana na ugonjwa huo tangu mwaka 2016 ni mmiliki wa kampuni ya Capital Group Limited inayomiliki kituo cha redio cha Capital FM.

Gazeti la Marekani la Forbes mnamo mwaka 2011 lilimuorodhesha wa pili kwa utajiri nchini Kenya nyuma ya familia ya hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Katika orodha ya utajiri barani Afrika, Dr. Chris Kirubi aliorodheshwa wa 31 kati ya watu 40.