Baraza la Magavana limetishia kusitisha utoaji wa huduma katika kaunti zote 47 wiki ijayo iwapo wizara ya fedha haitawapa shilingi billion 102.6 wanazodai.

Mwenyekiti wa baraza la Magavana Martin Wambora ametoa makataa ya hadi tarehe 24 mwezi huu kwa serikali kuwapa fedha hizo la sivyo wasitishe huduma zao.

Wambora aliye pia Gavana wa Embu anasema kutoka mwezi Aprili mwaka huu, serikali za kaunti hazijapata hela zozote kutoka kwa serikali kuu, hatua ambayo imelemaza shughuli ikiwemo kununua dawa.

Haya yanajiri licha ya waziri wa Hazina ya Kitaifa balozi Ukur Yatani kuziagiza serikali za kaunti kuwalipa wanakandarasi pesa zote wanazodaiwa.