Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amesema idadi ya wapiga kura iliongezeka na 149,600 tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Chebukati anasema hii inafikisha 19,678,885 idadi ya wapiga kura waliosajiliwa nchini kwa sasa.

Chebukati amesema haya alipoongoza shughuli ya kutoa hamasisho kwa wapiga kura ambayo imeanza rasmi na itachukua muda wa wiki moja katika maeneo bunge yote 290.

Tume hiyo inalenga kutumia mafunzo hayo pia kuelezea umma majukumu yake na mipango yao haswa kuhusu uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka ujao.

Hussein Marjan ni kaimu afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo.

Balozi wa Uingereza Jane Marriott aliyehudhuria shughuli hiyo amesema taifa lake litashirikiana na IEBC katika kuhakikisha kwamba uchaguzi huo mkuu unakuwa huru na haki.