Waziri wa Fedha Ukur Yatani ameliomba bunge kuruhusu deni la Kenya kupanda na kufikia Shilingi Trilioni Tisa (Sh9tr) ili kuwezesha kupatikana kwa Sh930b zinazohitajika kufadhili bajeti ya 2021/2022 inayogharimu Shilingi trilioni Tatu nukta Sita.

Waziri Yatani ameeleza kwamba bajeti hiyo iko juu kwa sababu ya majukumu mengi ambayo ni sharti serikali iwajibikie ikiwemo maendeleo.

INSERT: YATANI ON BUDGET

Balozi Yatani ameziagiza wizara zote sawa na serikali za kaunti kulipa madeni wanayodaiwa na wafanyibiashara kufikia Juni 30, 2021.

Mkate hautatozwa ushuru kuanzia Julai 1 kama ilivyokuwa imeratibiwa hii ikiwa ni afueni kwa wengi wa Kenya.

Idara mbalimbali zimetengewa pesa kama ifwatavyo:

*Serikali imetenga Sh14.3b kwa ununuzi wa chanjo dhidi ya corona

*Sh23b zimetengewa mpango wa kuwasaidia wasiojiweza katika jamii

*Mpango wa Kazi Mtaani umetengewa Sh1b huku shirika la KWS likipewa Sh1b, shirika la vijana NYS limetengewa Sh10b.

*Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta (KNH) imetengewa Sh15.2b huku ile ya rufaa ya Moi MTRH ikitengewa Sh11.5b.

*Utekelezwaji wa AJENDA NNE kuu za rais Uhuru Kenyatta umetengewa Sh142b.

*Sh500M zimetengwa kwa ajili ya kusaidia biashara mbalimbali

*Ujenzi wa nyumba nafuu umetengewa Sh8.4b huku ujenzi wa masoko ukitengewa Sh1b.

*Shirika linalosimamia Nairobi (NMS) limetengewa Sh27.2b ili kuendelea na majukumu yake.

*Awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Nairobi hadi Naivasha imetengewa Sh27.2b.

*Elimu imetengewa Sh202.8b; uajiri wa walimu ukitengewa Sh2.5b, vyuo vikuu vimepewa Sh76.3b huku vyuo vya mafunzo TVETS vikipewa Sh745M. Masomo ya bure katika shule za msingi yametengewa Sh12b huku shule za upili zikipewa 62.2b.

*Usalama ikiwemo idara ya Ulinzi na ujasusi NIS umetengewa Sh294.5b

*Sh15b imetengewa Michezo huku hazina ya CDF ikipewa 41.1b.

*Afisi ya mkurugenzi wa mkuu wa mashtaka ya umma (DPP) imepewa Sh3.2b, tume ya maadili na kupambana na ufisadi (EACC) imepewa Sh3.3b, idara ya upelelezi DCI Sh7.6b, mkaguzi wa hesabu za umma 5.9b, Bunge Sh37.9b na idara ya mahakama Sh17.9b.

*Wizara ya Afya imepewa Sh121b huku Kilimo ikipewa Sh60b, wizara ya Uchukuzi imepewa Sh182b.