Wakaazi wa Marakwet Magharibi wameamua kuchukua hatua za kuwakomesha wanafunzi wenye tabia ya kuzurura mitaani baada ya kutoka shuleni.

Akina mama wanasema wanafunzi hao huonekana wakizurura kwenye maduka na hata kujihusisha na tabia zisizofaa kama vile utumizi wa dawa za kulevya na ngono za mapema.

Badala ya kuenda moja moja hadi nyumbani baada ya kutoka shuleni, wanafunzi hao wanadaiwa kuranda randa katika masoko ya Kapsowar, Cheptongei, Chebara na Kapchenes.

Naibu kaunti kamishna wa eneo hilo Mathias Shishambo amewarai wazazi kuwapasha taarifa muhimu kama hizo zitakazosadia katika kuhakikisha kwamba wanafunzi hao wamekomeshwa.