Polisi huko Kericho wanamtafuta mwanafunzi wa shule ya Ainamoi anayedaiwa kumchapilia kichwani mwalimu wake mkuu na msumari wa nchi nne.

Mwanafunzi huo mwenye umri wa miaka kumi na nane anadaiwa kumpiga mwalimu wake na kibao kilichokuwa na msumari uliochomoza.

Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu anadaiwa kutekeleza kitendo hicho katika afisi ya mwalimu huyo alipoulizwa ni kwa nini hajamaliza kulipa karo.

Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo ana deni la shilingi elfu saba hajamaliza kulipa.

Mwalimu huyo Geoffrey Rono anaendelea kupokea matibabu huku uchunguzi ukianzishwa.