Mahakama imeendelea kumchapa rais Uhuru Kenyatta na mapigo zaidi baada ya kutaja kama kinyume cha katiba hatua yake ya kuweka idara ya mahakama chini ya usimamizi wake.

Jaji James Makau ametaja kama ukiukaji wa katiba hatua ya rais Kenyatta kufanya mabiliko ili idara ya mahakama na majopo kazi yake sawa na asasi huru za kikatiba kuwa chini ya afisi yake.

Tume ya huduma za mahakama (JSC), tume ya huduma za umma (PSC), tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu (KNCHR) pamoja na tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) zingeathirika na hatua hiyo ya rais.

Rais Kenyatta kwenye notisi ya Mei 11, 2020 alihamisha JSC pamoja asasi nyingine 39 chini ya afisi ya mwanasheria mkuu na mawaziri mbalimbali.

Hata hivyo chama cha mawakili nchini LSK kiliwasilisha kesi mahakamani kikitaja hatua hiyo kama inayokiuka katiba.