Zaidi ya wakimbizi 7,000 wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007/2008 kutoka kaunti za Nyamira na Kisii wameitaka serikali kuharakisha mpango wa kuwalipa fidia.
Wakizungumza nje ya mahakama ya Milimani wakati wa kutajwa kwa kesi yao, wakimbizi hao wakiongozwa na kasisi Nemwel Momanyi wamesema maisha yao yamebadilika tangu kutokea kwa ghasia hizo.
Aidha wameiomba mahakama kuharakisha kusikilizwa kwa kesi hiyo ndiposa wapate haki baada ya miaka 10 ya kungoja.
Wakimbizi hao wamelalama kwamba waliolipwa fidia awali hawakuwa wakimbizi halisi ila watu feki waliotumia ukora kupokea pesa kutoka kwa serikali wakijidai kuwa wakimbizi.