Rais Uhuru Kenyatta amesifia hatua ya Ethopia kuipa leseni kampuni ya mawasiliano ya Safaricom kuhudumu katika taifa hilo.
Rais Kenyatta amesema hatua hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa raia wa nchI hiyo sawa na kuimarisha uchumi.
Akitaja mafanikio ambayo Safaricom imekuwa nayo katika uchumi wa Kenya kwa miaka ya hivi karibuni, waziri mkuu wa Ethopia Abiy Ahmed ameelezea matumaini yake kwamba maazimio hayo pia yataafikiwa nchini mwake.
Rais Kenyatta alisafiri kwenda Ethopia kushuhudia kupewa leseni kwa Safaricom kuhudumu nchini humo.