Mtoto Shantel Nzembi aliyetekwa nyara na kisha mwili wake kupatikana Kitengela atazikwa Jumamosi hii katika kijiji cha Mawele kaunti ya Machakos.

Shantel mwenye umri wa miaka minane alitekwa nyara mwishoni mwa mwezi jana na mwili wake kupatikana umetupwa kando ya barabara ya Orata huko Kitengela.

Christine Ngina, mamake marehemu amesema maandalizi ya kumzika bintiye yanaendelea na familia imeamua kumzika nyumbani kwao.

Mahakama imeridhia ombi la kutaka washukiwa wa mauji hayo waendelee kuzuiliwa uchunguzi zaidi ukiendelea.