Kaunti ya Kisumu imeandiisha maambukizi mapya 129 ya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Kaunti hiyo iko kwenye darubini kufuatia msambao wa ugonjwa huo licha ya sherehe za Madaraka Dei mwaka huu kuandaliwa katika kauunti hiyo.

Kwa ujumla, Kenya imeandikisha visa 173,072 vya ugonjwa huo wa corona kufikia sasa.

Katika muda huo, taifa limeandikisha visa vipya 433 kati ya sampuli 4,479 huku kiwango cha maambukizi kikiwa katika asilimia 9.7%.

Wagonjwa 395 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 118 ,621 huku maafa mapya 18 yakiripotiwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 3,326.

Kufikia sasa, watu 1,005,509 wamepata chanjo ya corona huku waliopata dozi ya pili wakifikia 27,382.