Jaji mkuu Martha Koome ameunda jopo la majaji watatu kusikiliza kesi inayotoka kubatilishwa kwa uamuzi wa kumuondoa gavana wa Wajir Mohamed Mohamud Abdi.
Watatu hao ni Edward Muriithi, Patrick Jeremy Otieno na Thripsisa Cherere na watakuwa na kikao kwa njia ya kimtandao kesho asubuhi kutoa mwelekeo wa kesi hiyo.
Waliowasilisha kesi hiyo imahakamani ni Aden Ibrahim, Omar Jele, Bishar Ahmed, Safiya Mahammed na Yussuf Ibrahim na wanataka uamuzi huo kubatilishwa kwa sababu gavana Mohamud aliondolewa wakati ambapo kulikuwa na kesi mahakamani.
Wanaitaka mahakama kuamuru kwamba Mohamud bado ni gavana wa Wajir licha ya kuapishwa kwa naibu wake Ali Muktar kuwa gavana.