Amri ya waziri wa elimu Prof. George Magoha kwa walimu wakuu kwamba wanafunzi walipe karo ya muhula wa tatu inaendelea kuibua hisia mbalimbali.

Mbunge wa Matungu Peter Nabulindo amemkosoa Profesa Magoha akisema agizo hilo halikufaa ikizingatiwa kwamba wengi ya wazazi wanapitia ugumu wa kifedha wakati huu wa janga la corona.

Katika kutoa amri hiyo, waziri Magoha aliwalaumu baadhi ya wazazi walio na uwezo kwa kukosa kulipa karo wakitumia corona kama kisingizio.