Viongozi wa kisiasa kutoka eneo la Rift Valley wamekutana leo kupanga ajenda itakayopewa kipau mbele kwenye mazungumzo na naibu rais William Ruto.

Wakiongozwa na Gavana wa Turkana Josphat Nanok, wanasiasa hao ambao wamebuni kamati ya watu kumi na wanne kuangazia maslahi yao wamesema lengo lao ni kuhakikisha kwamba eneo hilo halibaki nyuma kimaendeleo.

Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amesema watapenya hadi mashinani kukusanya maoni ya wananchi kuhusu maswala wanayotaka yapewe kipau mbele.

Itakumbukwa kwamba viongozi kutoka eneo la Mt. Kenya wanashiriki kwenye mazungumzo kama hayo na Ruto katika kile wanasema ni kujumuishwa kwenye meza kuu wakati maendeleo yanajadiliwa.