Huku Ulimwengu ukiadhimisha Siku Ya Kimataifa Ya Usalama wa Chakula Jumatatu Juni 7, serikali imetoa hakikisho kwamba itamuwezesha kila Mkenya kupata chakula salama na cha kutosha.

Katika taarifa, waziri wa Kilimo Peter Munya amesema usalama wa chakula unafanikisha pakubwa biashara ya chakula na ni sharti ulindwe kwa vyovyote.

Waziri Munya amesema wizara yake iko macho kufuatilizia usalama wa chakula kuanzia shambani hadi kinapofika mezani.

Munya ametoa wito kwa kila mmoja kuhakikisha kwamba chakula kina usalama, kinapandwa kwa mazingira salama na umma kuelimishana kwa pamoja ili kuwa na ufahamu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi chakula.

Mada kuu ya mwaka huu ni ‘’Chakula salama sasa kwa afya ya kesho’’.