Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali yanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuonesha nia njema na kuwaapisha rasmi majaji sita waliosalia baada ya kuwaapisha wengine 34.
Katika taarifa, mashirika hayo yakiongozwa na mwenyekiti Suba Churchill yanasema ni kupitia kuapishwa kwao ndiposa watasafisha majina yao kufuatua madai ya maadili yaliyoibuliwa na rais.
Wanahoji kwamba kuapishwa kwao kutatoa nafasi kwa yeyote aliye na ushahidi kuuwasilisha kwa tume ya huduma za mahakama JSC na kisha uchunguzi kufanywa na ukweli kubainika.
Wameongeza kwamba kufikia sasa, sita hao Weldon Korir, Aggrey Muchelule, George Odunga, Joel Ngugi, Evans Makori na Judith Omange wamehukumiwa pasipo kupewa nafasi ya kujitetea.