Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kwa mara nyingine amewahimiza Wakenya kuwaripoti maafisa wa Polisi wanaochukua hongo ili kuwakinga wanaovunja sheria.
Akijibu maswali kuhusu kuongezeka kwa visa vya maafisa wa trafiki kuchukua hongo na kuruhusu matatu kubeba abiria kupita kiasi, Mutyambai amesema kupigana na ufisadi ni jukumu la kila mmoja na maafisa kama hao wataadhibiwa.
Mutyambai vile vile ametetea hatua ya Polisi kutibua mikutano ya kisiasa akisema mikutano hiyo inasalia kupigwa marufuku taifa linapokabiliana na janga la corona.
Inspekta wa Polisi wakati uo huo amesema kikosi maalum kimebuniwa kupambana na wahalifu wanaoibia watu katikati mwa jiji la Nairobi.