Mshukiwa mkuu kwenye mauaji ya mtoto Shantel Nzembi,8, aliyetekwa nyara na kisha kupatikana ameuawa atazuiliwa kwa saba zaidi

Mahakama ya Kajiado imeruhusu mshukiwa huyo Nativity Mutindi Nthuku kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kitengela kuwaruhusu Polisi kumaliza uchunguzi.

Mutundi,27, amefikishwa mbele ya Hakimu Mkaazi wa mahakama ya Kajiado Edwin Mulochi pamoja na mshukiwa wa nne Patrick Muriithi ambaye kadi ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake ilitumika kuitisha kikombozi kutoka kwa mamake msichana huyo.

Washukiwa walikuwa wanaitisha kikombozi cha Sh300,000.