Muungano wa majaji na mahakimu nchini KMJA umeelezea kushangazwa kwake na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kuacha nje majaji sita waliopendekezwa kuhudumu katika mahakama ya Rufaa.

Katika taarifa, katibu mkuu wa muungano huo Derrick Kuto amesema hatua ya Rais Kenyatta si tu kinyume cha katiba ya mwaka 2010 bali pia inaenda kinyume na maagizo ya mahakama.

Kuto anasema kwa mujibu wa katiba, Rais hana mamlaka ya kukataa kuteua majaji ambao wanapendekezwa kwake na tume ya huduma za mahakama JSC.

Muungano huo pia unasema Rais anaendelea kukiuka maagizo ya mahakama ambapo aliamrisha kuwateua majaji hao arobaine baada ya mmoja kufariki.

KMJA sasaiunamtaka Rais Kenyatta kuwateua mara moja sita hao waliosalia, ambao ni majaji Weldon Korir, Aggrey Muchelule, George Odunga na Joel Ngugi pamoja pia na Evans Makori na Judith Omange.