Mshukiwa wa nne kwenye mauji ya mtoto Shantel Nzembi ameshikwa katika eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado.

Mshukiwa huyo amekamatwa alikokuwa amejificha mjini Kitengela na majasusi waliokuwa wamevalia kiraia.

Marehemu Shantel alipotea baada ya kutekwa nyara wiki iliyopita na kisha mwili wake ukapatikana kwenye gunia siku chache baadaye.

Washukiwa wengine Livingstone Otengo na Francis Mikuhu walifikishwa mbele Hakimu Mkaazi Edwin Mulochi aliyekubali waendelee kuzuiliwa katika kituo cha Polisi ca Kitengela kwa siku 10 zaidi ili kufanikisha uchunguzi.