Kisumu imeandikisha visa vipya 145 kati ya maambukizi mapya 432 yaliyodhibitishwa nchini katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii ni baada ya kupima sampuli 3,800 idadi ambayo inafikisha jumla ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 171,658 huku kiwango cha maambukizi nchini kikipanda na kufikia asilimia 11.4%.

Aidha, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo katika kaunti ya Kisumu kimepanda na kufikia 34%.

Wagonjwa 17 zaidi wamefariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 3,223 huku waliopona wakifikia 117,345 baada ya kupona kwa watu 306 zaidi.

Jumla ya wagonjwa 1,227 wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku wengine 4,957 wakishughulikiwa nyumbani.

Walipata chanjo dhidi ya corona kwa mujibu wa wizara ya afya ni 972,601.