Maseneta wamekasirishwa na hatua ya Waziri wa mafuta na madini John Munyes kuwahepa na wametishia kumchukulia hatua iwapo atakosa kufika mbele yao tarehe kumi na nne mwezi huu.

Waziri Munyes anatakiwa kuelezea na kwa nini bei za mafuta zimekuwa zikipanda ama ashikwe.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge la Senate kuhusu Kawi Ephraim Maina amesema Munyes ametakiwa kuwaelezea maseneta kuhusu sababu za kupanda kwa bei za mafuta katika siku za hivi karibu.

Maseneta wameshangaa iweje mafuta yameendelea kuongezwa bei ilhali bei ya kuyasafirisha kuja huu nchini imerudi chini.