Aliyekuwa mbunge wa Kibwezi Richard Kalembe Ndile atazikwa Ijumaa ijayo ya Juni 11 nyumbani kwake Mbui Nzau, kaunti ya Makueni.

Mbunge wa Mavoko Patrick Makau ametangaza hili baada ya kuhudhuria mkutano wa kupanga safari ya mwisho ya mwenda zake.

Mbunge wa Kibwezi Magharibi Patrick Musimba atakuwa mwenyekiti wa kamati itakayosimamia mazishi ya mwendazake.

Ndile aliyefariki Jumapili iliyopita alihudumu kama mbunge kuanzia 2002 hadi 2007 na alifariki akipokea matibabu Nairobi Hospital.