Kaimu mkurugenzi katika wizara ya Afya Dkt. Patrick Amoth sasa ndiye mwenyekiti mpya wa bodi kuu ya shirika la afya duniani (WHO).
Haya yametangazwa na mtangulizi wake anayeondoka kutoka India Dkt. Harsh Vardhan wakati wa kikao cha 149 cha bodi ya utendaji ya shirika hilo.
Majukumu ya Dkt. Amoth ambaye amekaribisha uteuzi huo ni pamoja na kufanikisha utekelezwaji wa sera na maamuzi ya shirika hilo,
Dkt. Amoth atakayehudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja vile vile anatarajiwa kusimamia uchaguzi wa Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo katika kipindi chake.