Rais Uhuru Kenyatta ameilaumu mahakama kutokana na kile ametaja kama kuhitilafiana na demokrasia ya nchi hii kupitia baadhi ya maamuzi yake.

Akirejelea uamuzi wa mahakama kuu uliosimamisha mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI, rais amedokeza kwamba mahakama ilikosa kuzingatia kikamilifu umuhimu wa mchakato huo na uamuzi wa Wakenya wengi wanaotaka katiba kubadlishwa.

Rais Uhuru ameongeza taifa hili hupoteza pesa nyingi wakati wa misukosuko ya kisiasa kila baada ya uchaguzi.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishmiye ndiye alikuwa mgeni wa heshima kwenye maadhimisho hayoa ambayo pia yanahudhuriwa na naibu Rais William Ruto na aliyekuwa waziri MKuu Raila Odinga.