Naibu rais William Ruto ameisifia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyozinduliwa Kisumu na rais Uhuru Kenyatta kabla ya maadhimisho ya 58 ya Madaraka Dei.

Ruto amesema kuwa kuzinduliwa kwa miradi hiyo ni kiashirio tosha kuwa serikali inajitahidi kuwahudumia wananchi wake.

Naibu rais amesema haya wakati akiwahutubia Wakenya katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Jomo Kenyatta Jumanne ikiwa siku ya maadhimisho ya sikuu kuu ya Madaraka.