Mbunge wa Baringo Kusini Charles Kamuren ametoa wito kwa serikali kuharakisha kutoa pesa zilizofaa kutumika kujenga upya zaidi ya shule kumi zilizosombwa na mafuriko katika kaunti nne ikiwemo Baringo.

Mbunge huyo amesikitika kwamba ni mwaka mmoja sasa tangu serikali ilipoahidi kutoa Sh19.5b zilizotengwa na wizara ya elimu kwa minajili ya ujenzi huo ila kufikia sasa hilo halijafanyika.

Anasema kipindi hicho chote wanafunzi wamekuwa wakisomea chini ya miti ilhali pesa hizo zilifaa kufaidi shule kutoka Baringo, Pokot Magharibi, Elgeiyo Marakwet na Kisumu ambazo ziliathirika sana na mafuriko.