Jamaa watatu wameshitakiwa kwa kuiba faili za uchunguzi wa mauaji za mamlaka ya kumulika utendakazi wa Polisi (IPOA).

Watatu hao Nobert Ouko, Bernard Okello na David Okunda wanadaiwa kuiba faili hizo kutoka kwa makao makuu ya afisi za IPOA Mei 29.

Washukiwa hao vile vile wameshtakiwa kwa kukutwa na mali ya wizi mbele ya Hakimu David Ndungi.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kwamba washukiwa hao hawatakiwi kuachiliwa kwa dhamana kisa na maana huenda wakatatiza uchunguzi dhidi yao.

Licha ya kupinga ombi hilo kupitia kwa wakili wao, hakimu huyo amewanyima dhamana na kuagiza wazuiliwe kwa siku saba zaidi.