Mwelekeo kuhusu rufaa inayopinga uamuzi wa mahakama kuu kuhusu mchakato wa BBI utajulikana Jumatano wiki ijayo.

Rais wa mahakama ya rufaa Daniel Musinga ameziagia pande husika kufika mbele ya majaji watatu Jumatano saa tatu asubuhi kwa kikao cha pamoja.

Miongoni mwa yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho ni maombi yaliyowasilishwa mahakamani kuhusu uamuzi huo uliosimamisha marekebisho ya katiba kupitia BBI, tetesi zitakazowasilishwa na muda unaohitajika kwa pande husika kuwasilisha tetesi zao.

Ni wakili mmoja tu kutoka pande husika ataruhusiwa kuingia kwenye mahakama ambapo kikao hicho kitaandaliwa kwa sababu ya corona huku wenzake wakifuatilia kupitia kwa njia ya mtandao.

Waliowasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo ni rais Uhuru Kenyatta, kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na tume ya uchaguzi IEBC.