Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wameliongoza taifa katika maombi ya kitaifa yaliyofanyika katika majengo ya bunge.

Rais Kenyatta amewasihi Wakenya kuwa na matumaini licha ya changamoto zinazoletwa na janga la covid-19.

Rais Kenyatta vile vile amewataka wabunge na maseneta kupitisha mabadiliko mbalimbali katika sheria yaliyopendekezwa na serikali ili kuwezesha Wakenya kupata huduma bora za afya.

Matamshi yake yameungwa mkono na Naibu rais William Ruto ambaye amewataka wakenya kuweka Mungu mbele katika kila hali wanazopitia .

Ruto aidha amepigia debe kuanadliwa kwa mazungumzo ya kitaifa kutatua changamoto zinazolikumba taifa wakati huu.