Waziri wa afya Mutahi Kagwe anawasihi Wakenya kuwa makini kutokana na uwezekano kwamba aina ya virusi vya corona kutoka India na Uingereza vinasambaa katika jamii haswaa katika kaunti ya Kisumu.

Yanajiri haya wakati ambapo mtoto wa miezi miwili na ajuza wa umri wa miaka 101 wakiwa miongoni mwa watu 341 waliokutwa na virusi vya corona baada ya sampuli 3,646 kupimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Kufikia sasa jumla ya watu 169, 697 wamepatwa na virusi hivyo huku maambukizi yakiwa katika kiwango cha asilimia 9.4%.

Watu 144 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 115, 988 huku maafa 11 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa  3,108.

Kuhusu shughuli ya utoaji chanjo ya ya virusi vya corona inayoendelea kote nchini, jumla ya watu 963,241 wamepata chanjo hiyo ikiwemo wahudumu wa afya 164, 913, waalimu 151, 568, maafisa wa usalama 81, 309