Katika kutambua mchango wake kwa serikali na kaunti ya Nairobi, kutakuwa na barabara ambayo itaitwa Francis Atwoli.

Barabara hiyo iliyoko Kileleshwa karibu na shule ya Kenya High awali ilikuwa inaitwa Dik Dik Road.

Atwoli ambaye ametambua heshima hiyo chini ya uongozi wake kaimu gavana Ann Kananu amesema hilo limewezekana kutokana na juhudi zake kwa serikali na jamii kwa ujumla.

Katibu huyo mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU ameahidi kuendelea kumuunga mkono kikamilifu Kananu na uongozi wake.