Serikali imezindua mpango utaohakikisha kwamba wanaotafuta stakabadhi za uraia ikiwemo vitambulisho wanazipata chini ya kipindi cha siku 60.
Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i na katibu Karanja Kibicho wanasema kusudi kuu ni kupunguza mrundiko wa maombi 25,000 yanayosubiri kushughulikiwa.
Mpango huo unatazamiwa kuanza Juni 2 na kuendelea hadi Julai 31.
Mbali na vitambulisho, watakaoharakishiwa stakabadhi zao ni wale wanaotafuta uraia baada ya kuupoteza tangu mwaka 2010 wakati taifa lilipojipatia katiba mpya.