Mshukiwa mkuu wa mauaji ya aliyekuwa afisa wa mawasiliano katika tume ya ardhi nchini NLC Jennifer Wambua hayuko timamu kujibu mashtaka.

Mahakama imeambiwa kuwa uchunguzi wa kiakili umeonesha kuwa Peter Njenga almaarufu Sankala hana akili timamu.

Wakili wa mshukiwa Dorine Mwau ameiambia mahakama kuwa Sankala atafanyiwa ukaguzi mwingine wa kiakili tarehe 24 mwezi ujao.

Jaji wa mahakama kuu ya Machakos David Kemei ameagiza kesi hiyo kutajwa tena tarehe 22 mwezi ujao wa sita.