Mbunge wa Nakuru Magharibi Samwel Arama amepata pigo baada ya mahakama kuweka kando uamuzi uliokuwa umemuondoa lawamani kuhusiana na mashtaka ya ufisadi 2019.

Hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti Novemba mwaka 2019 alikuwa amefutilia mbali kesi dhidi ya mbunge huyo kwa misingi ya kukosekana kwa ushahidi.

Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika mahakama kuu na jaji James Wakiaga ameubatilisha.

Kesi hiyo inatazamiwa kutajwa Juni 15 kwa mwelekeo.