Muwaniaji wa chama cha People’s Empowerment (PEP) kwenye uchaguzi wa Kiambaa Raymond Kuria amekubali kumuunga mkono mwenzake wa United Democratic Alliance (UDA) John Njuguna Wanjiku.

Kuria amechukua uamuzi huu baada ya kukutana na naibu rais William Ruto siku moja baada ya chama hicho kinachohusishwa na mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kutangaza kujiondoa kwenye uchaguzi huo wa Julai 15.

Hatua ya Ruto inakinzana na ile ya chama chake cha Jubilee ambacho kimempa tiketi Karanja Kariri Njama kupeperusha bendera yake kwenye uchaguzi huo.

Kiti cha eneo bunge la Kiambaa kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge Paul Koinange.