Maambukizi mapya 382 ya ugonjwa wa corona ikiwemo mtoto wa miezi minne yameandikishwa nchini baada ya kupima sampuli 3,719 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Wizara ya afya inasema hii inafikisha 168,925 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini huku kiwango cha maambukizi kikipanda na kufikia 10.3%.
Katika muda huo, wamepona watu wengine 1,134 na kupandisha idadi ya waliopona kuwa 115,813.
Maafa yanayotokana na corona yameongezeka na kufikia 3,087 kufuatia kufariki kwa wagonjwa 14 zaidi huku wengine 113 wakiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU.
Watu 3,289 wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliochanjwa kuwa 957,804.