Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini (COTU) umepinga pendekezo la kuwataka waajiri kuwalipia wafanyikazi wao bima ya matibabu (NHIF) na wasiwakate kwenye mishahara yao.

Marekebisho kwenye mswada wa NHIF uliowasilishwa bungeni na kiongozi wa walio wengi Amos Kimunya unapendekeza waajiri kulipa faini iwapo watashindwa kuwalipia wafanyikazi wao pesa hizo.

Hata hivyo COTU kupitia kwa taarifa inasema mswada huo utasababisha kuvunjwa kwa NHIF na kuundwa kwa bodi nyingine ambayo haitakuwa na umuhimu kwa mfanyikazi.

Ilivyo kwa sasa, wafanyikazi wanajilipia NHIF kwa hiari na waajiri wanajukumika kulipa ada hizo na kisha kukata kwenye mishahara ya wafanyikazi.