Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kuongoza maombi ya kitaifa Alhamisi hii kutoka majengo ya bunge.

Rais ataandamana na viongozi mbalimbali ikiwemo maspika wa mabunge yote mawili, jaji mkuu na viongozi wengine wa kisiasa na kidini.

Hii itakuwa ni hafla ya kumi na nane tangia kuanza kuadhimishwa kwa maombi ya kitaifa.

Maombi sawia na hayo mwaka uliopita yalifanyika katika ikulu ya Rais Nairobi, siku chache baada ya Kenya kuripoti kisa cha kwanza cha corona.