Maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini yako katika kiwango cha asilimia 5.7% huku visa vipya 111 vikipatikana kati ya sampuli 1,948 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 168,543 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa kwa mujibu wa wizara ya afya.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 114,679 baada ya watu 142 kupona katika muda huo wa siku moja.

Maafa yamefikia 3,073 baada ya kufariki kwa wagonjwa 15 zaidi huku waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ICU ikiwa 121.

Kufikia sasa idadi ya waliopata chanjo dhidi ya ugonjwa huo ni 954,515.