Polisi watatu wameuawa Ijumaa baada ya gari lao aina ya Land Cruiser kukanyaga kilipuzi cha kutegwa ardhini katika barabara kuu ya Banisa-Tabaka kaunti ya Mandera.

Maafisa hao walikuwa wanashika doria wakati walivamiwa na watu wanaoaminika kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Alsha baab na kuwajeruhi baadhi ya maafisa hao.

Gari hilo lilikuwa limebeba Polisi kumi na tano waliokuwa kwenye doria.

Duru zaarifu kuwa kulikuwa na hali ya ufyatulianaji wa risasi baina ya Polisi na wanamgambo hao ambao walitorokea kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.

Oparesheni kali imeanzishwa katika eneo hilo kuwatafuta washukiwa zaidi.