Hatimaye jaji Mkuu Martha Koome ameapishwa rasmi kuanza majukumu yake kwenye hafla iliyoandaliwa katika Ikulu ya rais jijini Nairobi.

Koome ambaye ameandikisha historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo amekula kiapo kwenye hafla iliyohudhuriwa na rais Uhuru Kenyatta na mwanasheria mkuu Kihara Kariuki.

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuendelea kushirikiana na idara ya mahakama kuhakikisha kuwa mchakato wa kupatikana kwa haki umefaulu.

Aidha, jaji William Ouko ameapishwa kukuwa jaji wa mahakama ya upeo kuchukua wadhifa uliowachwa wazi na Jacktone Ojwang’ aliyestaafu.

Kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu kustaafu kwa David Maraga kuanzia Januari 12, 2021 atamkabithi rasmi mikoba Koome Jumatatu ijayo.